Joto la pambano la kugombea kucheza nusu
fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya ndani ya dimba la Santiago
Bernebau linazidi kupamba moto, na Real Madrid wanaingia kwenye mechi hii wakiwa ndio timu iliyocheza robo fainali nyingi kuliko timu zote kwenye historia ya ligi ya mabingwa wa ulaya - wakicheza mara 30, na sasa wapo kwenye pambano la kuweza kucheza nusu fainali yao ya 24 katika historia yao ndani ya Champions league.
Sio tu Madrid watakuwa wanapewa sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki wao wanaofikia 80,000
kwenye mechi hii ya kwanza, lakini pia namba zinawapa nafasi Los
Blancos: timu hii ikiongozwa na Jose Mourinho imeenda miezi 14 bila
kupoteza mechi kwenye dimba lao la nyumbani kwenye michuano ya ulaya.
Lakini bado haitakuwa rahisi, Galatasary, wakiwa wanaongoza ligi ya Uturuki wamekuwa na rekodi ya kushinda mechi tatu za ugenini kwenye Champions league.
0 comments:
Post a Comment