Popular Post

Home » » TIGER WOODS AVUTA KIFAA KIPYA.

TIGER WOODS AVUTA KIFAA KIPYA.

NYOTA namba moja wa zamani duniani katika mchezo wa gofu, Tiger Woods na bingwa wa michuano ya olimpiki ya kuteleza kwenye barafu wa Marekani Lindesey Vonn wametangaza rasmi kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Wawili hao walitangaza taarifa hizo katika kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo walituma picha wakiwa pamoja na kumaliza uvumi uliokuwa umesambaa juu ya mahusiano yao. Woods amewahi kumuoa mwanamitindo kutoka Sweden Elin Nordegrem lakini walitalikiana mwaka 2010 baada ya nyota huyo tajiri kukiri kuwa na mahusiano na wanawake mbalimbali akiwa ndani ya ndoa yao. Woods mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akihangaika kurejea katika kiwango chake toka kipindi hicho na sasa ameanza kuonyesha dalili za kurejesha makali yake ambayo yalimfanya atawale mchezo wa gofu kwa muongo mmoja.
Share this video :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2013. Team Rashid Blogspot . - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger